Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi anasubiri tuzo yake ya Kocha bora wa Ligi Kuu na kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) msimu huu
Nabi amedhihirisha ubora wake pasipo na shaka kwa kuiongoza Yanga kushinda mechi nyingi kutokana na umahiri wake wa kusoma mchezo
Msimu huu Yanga imekuwa na kawaida ya kupata ushindi kwenye kipindi cha pili kutokana na umahiri wa Nabi katika kufanya 'sub'
Singida BS waliamini wameimudu Yanga lakini dakika 15 za mwisho Nabi akawaduwaza katika uwanja wao!
Kennedy Musonda, Fiston Mayele na Tuisila Kisinda wakaingia na bao lililoipeleka Yanga fainali ya FA
Nabi ameipa Yanga Ngao ya Jamii, Ligi Kuu, ameipelekea Yanga fainali mbili za FA na Shirikisho CAF
Huko mtaani wanasema ukiona Nabi anafanya 'sub' kuwa makini ni mtego huo!