Tutapambana tupate ushindi Jumapili - Job

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 May 2023
Tutapambana tupate ushindi Jumapili - Job

Mlinzi wa Yanga Dickson Job amesema ni ndoto ya kila mchezaji kucheza fainali ya mashindano ya CAF hivyo hiyo ni nafasi kwao, watapambana kuhakikisha wanaibuka na ushindi na kuwa mabingwa wa kombe la Shirikisho barani Afrika

Jumapili May 28 Yanga itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili USM Alger katika mchezo wa fainali kombe la Shirikisho barani Afrika

Job amesema wameendelea vyema na maandalizi yao akiwataka mashabiki wa Yanga na Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumapili ili kuwapa sapoti

"Walimu wameleta mfumo ambao tutahitaji kuutumia katika mchezo huo. Sisi kama wachezaji tumeupokea na tutahakikisha tunautimiza kwa asilimia 100 ili tuweze kushinda mchezo huo"

"Tutapambana kwa asilimia 100 ili kupata matokeo mazuri katika mchezo huo wa mkondo wa kwanza katika uwanja wetu wa nyumbani"

"Kikubwa niwaombe Wananchi na Watanzania wote waje kwa wingi kutuunga mkono katika mchezo huo. Tunawaahidi tutawapa furaha," alisema Job

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’