Washambuliaji wa Yanga Fiston Mayele na Kennedy Musonda wameitwa katika timu za Taifa DR Congo na Zambia kwa ajili ya mechi za kuwania kufuzu Afcon 2023
DR Congo itacheza na Gabon Juni 18 wakati Zambia itachuana na Ivory Coast Juni 17

Nyota zaidi wa Yanga wanatarajiwa kupokea wito kwa ajili kwenda kuyatumikia Mataifa yao kwa ajili ya mechi za kuwania kufuzu Afcon 2023
Djigui Diarra, Stephane Aziz Ki, Khalid Aucho ni miongoni mwa wachezaji wanaotarajia kujumuishwa katika timu za Taifa
Kwa upande wa Tanzania nyota ambao wana nafasi ya kuitwa timu ya Taifa ni pamoja na Metacha Mnata, Bakari Nondo Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Dickson Job, Kibwana Shomari, Mudathir Yahya, Clement Mzize na pengine Salum Abubakar 'Sure Boy'
Tanzania itachuana na Niger Juni 18 katika uwanja wa Benjamin Mkapa