Serikali yakamilisha safari ya Yanga Algeria

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 May 2023
Serikali yakamilisha safari ya Yanga Algeria

Serikali imeeleza kukamilisha mipango yote kwa ajili ya safari ya Yanga kuelekea Algeria kwenye mechi ya fainali ya mkondo wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger.

Mchezo huo wa pili unatarajia kuchezwa Juni 3, mwaka huu Uwanja wa Julai 5, 1962 mjini Algiers baada ya USMA kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam juzi Jumapili.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa alisema kama ahadi ilivyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan, ametekeleza kwa kutoa ndege yenye uwezo wa kubeba abiria 262 kuipeleka timu hiyo kesho Alhamisi na kurejea Juni 4, mwaka huu baada ya mechi hiyo

"Kama ilivyotangazwa, Rais ametoa ndege ambayo ina uwezo wa kubeba abiria 262 kwa ujumla wake lakini pengine mwongozo utatolewa hapo baadaye, lakini maelekezo ya Rais Samia anahitaji ibebe wachezaji, viongozi na mashabiki wa kwenda kushangilia," alisema Msigwa

Alisema matokeo ya mechi ya kwanza hayakuwa mazuri lakini Serikali imetekeleza wajibu wake kuhakikisha wanaondoa uchovu kwa safari ambapo ndege hiyo itaruka moja kwa moja mpaka Algiers ikitumia saa tano mpaka sita

Alisema serikali inaamini kupitia Yanga kwamba inaweza kuuleta ubingwa huo nchini msimu huu, ndiyo maana inashirikiana nayo kuhakikisha wanatimiza ndoto yao hiyo

Wakati huo huo, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoa pole kwa familia iliyopoteza mpendwa wao, William Ernest aliyefariki katika mchezo wa kwanza wa fainali hiyo kwenye Uwanja wa Mkapa

Wizara pia ilitoa pole kwa majeruhi wengine katika tukio hilo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara, inamwombea marehemu apumzike kwa amani na majeruhi wengine wapone haraka na warejee katika majukumu yao ya ujenzi wa taifa

"Tunatoa pole kwa wafiwa na Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahala pema peponi, lakini pia tunaombea kwa Mungu majeruhi wote wapone warejee kwenye shughuli zao za ujenzi wa Taifa," ilisomeka taarifa hiyo ya Wizara.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’