Twendeni tukamalize kazi iliyobaki - Arafat

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Jun 2023
Twendeni tukamalize kazi iliyobaki - Arafat

Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amesema umoja na ushirikiano wa Wanayanga umewezesha kufikia mafanio ambayo hakuna aliyetarajia katika mashindano ya CAF msimu huu

Saa 4 usiku Yanga itashuka uwanja wa July 05 huko Algeria kumenyana na USM Alger katika mchezo wa pili wa fainali kombe la Shirikisho barani Afrika Yanga ikihitaji ushindi wa angalau mabao mawili ili kushinda taji

Arafat amesema kazi kubwa imefanyika mpaka Yanga kufika hapo ilipo, kwa pamoja leo wanakwenda kumalizia kazi iliyobaki

Kupitia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Arafat ameandika ujumbe huu;

"Wananchi wenzangu leo tuna mechi muhimu katika historia ya klabu yetu. Sisi tupo hapa Algiers, Algeria tunawakilisha mamilioni ya wananchi wengine wengi duniani kote.

Wakati wote umoja wetu ndio umekuwa silaha na nguzo yetu, wananchi tuendelee kuwa pamoja na timu yetu kwa sala na dua kuelekea mchezo wetu wa hapo baadae.

Wakati watu wote wakiamini tusingeweza kufuzu hatua ya makundi baada ya kupangwa na timu kutoka Tunisia, lakini wananchi tuliamini inawezekana na tulifanikiwa.

Wakati wengine wakiamini tusingeweza kufuzu hatua ya Robo Fainali mbele ya vigogo TP Mazembe na US Monastir lakini sisi Wananchi tuliamini inawezekana na tukaongoza kundi.

Tukaambiwa mwisho wetu utakuwa Robo Fainali lakini sisi tuliamini tunaweza kusogea zaidi ya hapo na tukafanya hivyo!

Bado tukaambiwa mwisho wa safari yetu utakuwa Nusu Fainali lakini wananchi tuliamini tunakwenda hadi Fainali na leo tupo hapa.

Hadi leo kuna ambao wanaamini Wananchi hatuwezi kuchukua ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika lakini sisi wenye timu tunaamini Kombe linarudi nyumbani Tanzania.

Wananchi twendeni tukamalizie kipande kilichobaki cha kuchukua ubingwa"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
4h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
22h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’