Wachezaji Hassani Kessy na Emanuel Martin leo hawamo katika kikosi cha kwanza cha Yanga kinachoikabili Stand United, lakini wapo miongoni mwa wachezaji wa akiba.
Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina leo amempa nafasi ya kuanza winga Yusuph Mhilu baada ya kuridhishwa na kiwango alichoonyesha kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar Ijumaa iliyopita.
Beki wa kulia Juma Abdul naye amerejea katika kikosi cha kwanza kuchukua nafasi ya Hassani Kessy aliyepumzishwa.
Hata hivyo huenda kocha Lwandamina anamuandaa Abdul kwa ajili ya mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers March 17 kwa kuwa Kessy hatacheza mchezo huo akitumikia adhabu ya kadi mbili za njano.
Naye kiungo Thabani Kamusoko aliyerejea kikosini Ijumaa iliyopita leo hakupata nafasi ya kuanza lakini huenda akapata dakika kadhaa za kucheza ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kurejesha makali yake baada ya kuwa nje kwa muda mrefu kutokana na majeruhi.
Raphael Daudi hakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichoivaa Kagera Sugar kwa kuwa alikuwa akitumikia adhabu ya kadi tatu za njano lakini leo Lwandamina amemrejesha kikosini.
Kiungo Papi Tshishimbi imeelezwa ana matatizo ya kiafya na leo anakosa mchezo wa pili mfululizo lakini huenda akarejea kikosini Yanga itakapoikabili Township Rollers Jumamosi ijayo

ADVERTISE HERE