Bodi ya Ligi yateta na timu zinazoshiriki Kimataifa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Jun 2023
Bodi ya Ligi yateta na timu zinazoshiriki Kimataifa

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imekutana na Wakurugenzi Watendaji wa klabu nne zilizopata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa ya CAF ili kupanga mikakati ya namna gani zijipange kuelekea msimu mpya wa mashindano yao

Timu hizo ambazo ni Yanga, Simba zitakazoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, Azam FC na Singida Fountain Gate kwenye Kombe la Shirikisho Afrika pamoja na Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)Β 

Mabosi hao walikutana kuona namna gani ratiba yao ilivyo na kuwashauri jinsi ya kusajili vikosi vipana na kujiandaa vyema kutokana na namna miundombinu ilivyo nchini wanapokwenda kucheza mechi za ugenini

Afisa Mtendaji Mkuu wa TPLB, Almasi Kasongo alisema timu hizo zinatakiwa kujiandaa vizuri kwa mambo mawili, kiuchumi na usajili

"Miundombinu yetu sio rafiki sana, hivyo hawa wawakilishi wetu wanapaswa kujiaandaa vizuri sana kuanzia uchumi hadi usajili wao, wawe na vikosi vipana maana ratiba inaweza kuwabana, wakatoka kucheza nje ya nchi halafu wakifika hapa wanakuwa na mechi za nje ya mikoa yao"

"Hivyo kuna kila sababu ya kujipanga vizuri kwao kwneye mambo hayo mawili na tutajitahidi kutengeneza ratiba ambayo itakuwa rafiki kwa timu zote ili pia kuepukana na mechi za viporo," alisema Kasongo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
5h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’