Taasisi ya Mwamnyeto Foundation ambayo imeanzishwa na wachezaji wawili wa Yanga, Bakari Mwamnyeto na Zawadi Mauya, imeandaa matamasha mawili yatakayofanyika katika mikoaya Tanga na Morogoro
Lengo la matamasha hayo ni kutoa misaada mbalimbali na kurudisha kwa Jamii
Tamasha la kwanza litafanyika Julai 2, 2023 mkoani Tanga ambako Mwamnyeto anatokea na tamasha la pili litafanyika Julai 7, 2023 mkoani Morogoro ambako ni nyumbani kwa Mauya
Matamasha yote mawili yatahusisha mambo mawili, jambo la kwanza ni kutembelea vituo vya watu wenye uhitaji maalum halafu jambo la pili itakuwa ni mechi ambayo itahusisha timu itakayoundwa na Mwamnyeto na Mauya na watu wao dhidi ya combine ya Mkoa wa Tanga pamoja na Morogoro
ADVERTISE HERE