Kocha wa Yanga, Mzambia George Lwandamina, amesema katika mchezo wa Jumamosi wa marudiano wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers, hawatawapa nafasi wapinzani wao kumiliki mpira.
Kikosi cha Yanga kikiwa na wachezaji 20 na viongozi 11 wakiwemo saba wa benchi la ufundi walioondoka nchini alfajiri ya jana kuelekea Botswana tayari kwa mchezo huo wa marudiano.
Akizungumza muda mfupi kabla ya safari, Lwandamina alisema kuwa walikosea kwenye mchezo wa kwanza ambao Yanga walilala kwa mabao 2-1 kwa kuwapa nafasi wapinzani wao hao kumiliki mpira na kupata nafasi ya kujipanga.
"Unapomiliki zaidi mpira unapata nafasi ya kupanga mashambulizi na kutafuta nafasi.., tunaenda kwenye mchezo wa marudiano tukiwa tayari tumefanya marekebisho kwenye eneo ambalo tuliteleza," alisema Lwandamina na kuongeza, "Wachezaji wangu wapo kwenye ari nzuri, tutapambana mpaka dakika ya mwisho," alisema.
Alisema hawatacheza soka la kujilinda na badala yake watajitahidi kuwashambulia ili kuwapa presha wapinzani hao.
"Tukifanikiwa kupata bao kwenye kipindi cha kwanza itatupa kasi zaidi na ndicho tunachotaka kufanya, tupo nyuma kwa mabao 2-1 hivyo hakuna sababu ya 'kupaki basi'," alisema Lwandamina.

ADVERTISE HERE