Yanga kufungua Tawi Malawi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Jul 2023
Yanga kufungua Tawi Malawi

Klabu ya Yanga imeridhia kufunguliwa kwa Tawi la Wanachama nchini Malawi

Jana baada ya Yanga kuwasili Malawi, miongoni mwa waliojitokeza kuwapokea mabingwa hao wa Tanzania Bara ni mashabiki wa Yanga waishio huko Malawi

Mashabiki hao wakawasilisha ombi lao la kufunguliwa Tawi kwa Rais wa Yanga Injinia Hersi Said ambaye aliagiza mchakato wa kufunguliwa tawi hilo uanze mara moja

"Tumefurahi kuona hapa Malawi Yanga ina mashabiki wengi sana, ombi lenu la kufunguliwa Tawi hapa tumelipokea na nimewaagiza vijana wangu waanze mchakato huo mara moja"

"Nimewaambia hapa mko watu 300, mnaweza kujisajili kuwa Wanachama wa Yanga kupitia simu janja, mkifikisha idadi ya Wanachama 100 basi Tawi lenu litatambulika"

"Kwa mujibu wa Katiba yetu, Tawi hai lenye Wanachama kuanzia 100 linaruhusiwa kutoa Wawakilishi kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama hivyo nanyi Wanayanga wa Malawi mtaweza kushiriki kwenye Mkutano huo kutoa maoni yenu"

"Tunapenda kuona Yanga inakuwa na Wanachama sio hapa Malawi tu, bali iwe dunia nzima," alisema Hersi

Jioni ya leo Yanga itashuka dimba la Bingu kumenyana na Nyasa Big Bullets katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki katika maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Malawi

Takribani mashabiki 41,000 wanatarajiwa kushuhudia mchezo ambao pia utashuhudiwa na Rais wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake Rais wa Malawi Lazarus Chakwera

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’