Namba 6 ataitikisa nchi - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Jul 2023
Namba 6 ataitikisa nchi - Kamwe

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema utambulisho wa kiungo Jonas Mkude sio yule namba sita ambaye wamemzungumza kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa

Kamwe amesema namba sita atakuwa mchezaji wa mwisho kutambulishwa siku ya Jumanne ambapo amebainisha kuwa utambulisho wake utaitikisa nchi

"Tutamtambulisha saa 6 na dakika 6 usiku, tunataka tukio hili liwe kama sherehe za maadhimisho ya Mwaka mpya"

"Baada ya utambulisho wake mashabiki wa Yanga wataingia mtaani kusherehekea ujio wa mchezaji huyu mkubwa lakini pia kuna watu watajifungia ndani wakiwa na huzuni"

"Yaani siku hiyo kwa furaha ambayo Wananchi watapata, mafataki yatapigwa, ngoma zitapigwa, nyimbo zitaimbwa kila pande ya nchi hii watu watafurahi"

"Baada ya utambulisho wake, kesho yake asubuhi atakuwa hapa Makao Makuu ya CRDB ambao mashabiki wa Yanga watapata nafasi ya kuwa wa kwanza kupiga nae picha baada ya kujiunga kuwa Wanachama au kulipia kadi zao za uwanachama au shabiki," alisema Kamwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
6h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’