Kiungo Jonas Mkude ni miongoni mwa wachezaji waliotua Yanga katika dirisha hili la usajili akitokea klabu ya Simba
Usajili wake ulikamilishwa baada ya Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa Tanzania Bara kwa misimu miwili mfululizo Miguel Gamondi kuidhinisha
Katika mapendekezo yaliyoachwa na aliyekuwa Kocha Mkuu Nasreddine Nabi ni pamoja na maboresho katika eneo la kiungo
Uwepo wa Mkude sokoni uliwafanya mabosi wa Yanga wasione sababu ya kwenda nje ya nchi kutafuta kiungo kwani katika ubora wake, Mkude ni kiungo wa daraja la juu
Wanaomhukumu wanaangalia historia yake na Simba katika msimu uliopita. Wengi wanadhani kwa kuwa hakuwa akipata nafasi Simba basi kiwango chake kimeshuka
Wako watu watasubiri akosee ili washushe lawama, hivyo mwenyewe anafahamu, hii ni nafasi yake adimu kuwajibu kwa vitendo
Mkude hatakuwa mchezaji wa kwanza kuwafunga midomo wale wanaokuwa na mashaka, ilikuwa hivyo kwa Salum Abubakar, wengi waliona kama Yanga imepata hasara kwa kumsajili Sureboy kutoka Azam Fc
Hata Mudathir Yahya usajili wake kutoka Azam Fc ulikumbana na maswali mengi, lakini miezi yake sita imetosha kuwanyamazisha wakosoaji wake