Baada ya uzinduzi uliofana hapo jana, Documentary ya Yanga itaanza kupatikana leo kuanzia saa 10 jioni katika App ya Azam Max (Azam Media)
Mwananchi unapaswa kuiona Documentary hii ili kufahamu mengi ambao hukupata kuyafahamu katika mapambano ya Yanga msimu uliopita
Ulikuwa ni msimu wa furaha kwa Yanga kushinda mataji yote pamoja na kucheza fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika lakini ziko nyakati ngumu ambazo zilipitiwa katika kuisaka furaha ya Wananchi
Gharama ya kuishuhudia Documentary hiyo ni Tsh 2,500/- tu. Usisubiri kuhadithiwa, hakikisha umeiona ili uchangie timu yako pia





ADVERTISE HERE