Klabu ya Yanga leo imeingia makubaliano ya ushirikiano na kituo cha kukuza vipaji Moro Kids kutoka mkoani Morogoro
Ushirikiano huo utashuhudia Yanga ikisimamia masuala mbalimbali kama kujenga uwezo kitaaluma, vifaa vya michezo, uwezeshaji wa kiuchumi na kubadilishana uzoefu
Yanga pia itawajibika kuwatafutia soko wachezaji wanaozalishwa na kituo hicho
Yanga ni miongoni mwa timu zilizonufaika na wachezaji kutoka kituo hicho. Ushirikiano huo utaifanya Yanga kuwa daraja kwa vijana wenye vipaji kutoka mkoani Morogoro
Kibwana Shomari, Nickson Kibabage, Dickson Job na Aboutwalib Mshery ni miongoni mwa wachezaji waliowahi kupita katika kituo hicho


ADVERTISE HERE