Historia imeandikwa katika soka la Tanzania kwani kwa mara ya kwanza Kocha Mwanamke amekabidhiwa majukumu ya kuinoa imu ya Wanaume
Ni aliyekuwa kocha wa Yanga Princess Edna Lema ambaye jana alitangazwa kuwa kocha msaidizi wa Biashara United inayoshiriki Championship. Lema amepewa mkataba wa mwaka mmoja
"Imekuwa ndoto yangu ya muda mrefu kufundisha soka la wanaume na hatimaye leo inaenda kutimia, kwangu inaenda kuwa changamoto mpya. Ingawa haitokuwa jambo rahisi lakini nipo tayari"
"Mkataba wangu ni wa mwaka mmoja na jukumu letu kubwa pamoja na hamu ya wanamara ni kuhakikisha klabu ya Biashara inarejea kwenye ligi kuu Tanzania Bara," aisema Edna
Edna alikinoa kikosi cha Yanga Princess kwa misimu mitatu, msimu wake wa mwisho ukiwa 2021/22 akiisaidia Yanga Princess kumaliza nafasi ya pili kwenye msmimamo wa ligi ya Wanawake ikitofautiana na Simba Queens waliokuwa mabingwa kwa tofauti ya alama moja tu
Lema anakamilisha mafunzo ya Leseni A ya CAF ambayo itamuwezesha kufundisha timu za Ligi Kuu na hata nje ya nchi