Ni msimu mwingine wa michuano ya Kimataifa ambapo mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga watakuwa uwanja wa Azam Complex kuikabili Asas Fc katika mchezo wa kwanza wa hatua ya awali michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Baada ya Asas Fc kukosa uwanja unaokidhi vigezo vya CAF, klabu hiyo imelazimika kucheza mechi yake ya nyumbani kwenye uwanja wa Azam Complex
Historia iliandikwa na Yanga msimu uliopita kwa kucheza fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Wananchi wana shauku kubwa ya kuona kile kilichofanyika katika kombe la Shirikisho kinarudiwa msimu huu katika ligi ya mabingwa
Ni mwanzo wa safari ya Yanga kuelekea hatua ya makundi, baada ya kukosa kucheza hatua hiyo kwa zaidi ya miaka 24
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema leo wataitumia Asas Fc kuwatumia ujumbe wengine kuwa Yanga imedhamiria kufanya makubwa msimu huu
Mchezo utapigwa kuanzia saa 11 jioni..