Bado hatujamalizana na Asas Fc - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Aug 2023
Bado hatujamalizana na Asas Fc - Kamwe

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amewataka Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanja wa Azam Complex siku ya Jumamosi, August 26 katika mchezo wa mkondo wa pili ligi ya mabingwa barani Afrika hatua ya awali dhidi ya Asas Fc

Kamwe amesema wanahitaji kushinda mchezo huo ili kujihakikishia tiketi ya kutinga raundi ya kwanza ya michuano hiyo ikiwa ni hatua moja kuelekea makundi

"Mchezo huu haujamalizika kama wengi wanavyosema. Unapodharau mpinzani kwa sekunde moja tu, mechi inaweza kubadilika. Iko mifano mingi tu, kuna timu ziliwahi kushinda ugenini na kupoteza nyumbani"

"Kwa kuwa tuna dakika 90 za kucheza hatupaswi kuwadharau wapinzani wetu. Tunaomba mashabiki wetu mje kwa wingi kushangilia ili kuhakikisha tunasonga mbele. Nawaomba mashabiki tusiingie katika mtego wa kudhani mechi imemalizika"

Kamwe ametangaza viingilio vya mchezo huo ambapo Mzunguuko ni Tsh 5,000/-, VIP B ni Tsh 20,000/- naΒ VIP A ni Tsh 30,000/-

Kamwe amewaasa mashabiki kuhakikisha wananunua tiketi zao mapema, wasisubiri kukata tiketi uwanjani kwani kuna matukio ya kuuziwa tiketi feki

Aidha Kamwe amesema siku hiyo imepewa jina la 'Max Day', Wananchi wataitumia kumuenzi mchezaji wao Max Nzengeli kwa kuchomekea

"Kwa yeyote atakayekuja uwanjani ahakikishe amechomekea, huu ndio utakuwa mtoko wetu wa Max Day," alisema Kamwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
37m ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
55m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
18h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’