Yanga yazindua huduma za kidigitali

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Mar 2018
Yanga yazindua huduma za kidigitali
Ifikapo April 01, 2018 klabu ya Yanga itaanza rasmi kipindi chake cha televisheni kupitia runinga ya Azam kitakachojulikana kwa jina la 'Yanga TV Show'.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo, Mwakilishi wa Televisheni wa Azam FC Baruani Muhuza amesema kipindi hicho kitakuwa tofauti na vipindi vingine vya klabu kama Simba TV na Azam TV kwa kuwa kitaandaliwa na kuendeshwa na WanaYanga wenyewe.

Awali Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa alisema Yanga imeamua kuja na mfumo huo wa kidigitali ili isogee karibu ya wanachama na mashabiki wake popote walipo.

Mbali na Yanga TV, huduma ya kupata habari mbalimbali za Yanga kupitia ujumbe mfupi kwenye simu za mkononi imezinduliwa.

Huduma hiyo kwa sasa inapatikana kwenye mtandao wa Tigo ambapo ili uweze kujiunga unatuma neno YANGA kwenda 15501.

Gharama ya ujumbe mfupi ni Tsh 100 tu.

Kwa kujiunga na huduma hiyo, licha ya kupata habari 'za motomoto' kutoka klabu ya Yanga, pia utakuwa umeichangia timu yako.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
25m ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
4h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
22h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’