Kiungo wa Yanga, Mudathir Yahya ni wamoto kwelikweli msimu huu akijihakikishia nafasi kwenye kikosi cha Kocha Miguel Gamondi
Katika mechi za mashindano, Mudathir alikosa mchezo mmoja tu dhidi ya Asas Fc ukiwa ni mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa hatua ya awali
Usajili wake uliofanyika msimu uliopita katika dirisha dogo ulionekana wa kawaida sana lakini wengi wakashangazwa na kile alichofanya katika miezi sita aliyotumika chini ya aliyekuwa kocha wa Yanga Nasreddine Nabi ambaye alipendekeza asajiliwe baada ya Feisal Salum kujiengua Yanga
Msimu huu Mudathir amekuwa bora zaidi; yeye na Khalid Aucho wakiwa chaguo la kwanza katika eneo la kiungo katika kikosi cha Gamondi
Mudathir anatumika kama kiungo huru 'box-2-box' ambaye anakuwa kwenye eneo la ulinzi timu inaposhambuliwa na kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji. Mpaka sasa ana bao moja katika ligi kuu ya NBC
Mudathir ni mfano wa wachezaji wa ndani ambao wamefanikiwa kupenya na kupata nafasi na kuaminiwa mbele ya wachezaji wa kigeni
Yanga imejipambanua kwa kuwa na wachezaji wengi wa ndani ambao wana viwango bora na wamejihakikishia nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza
Akielekea kwenye majukumu ya timu ya Taifa, pasipo na shaka Mudathir huko katika mchezo dhidi ya Algeria, ataendeleza ubora wake