Droo ya makundi ya michuano ya CAF, ligi ya mabingwa sambamba na raundi ya mwisho ya mtoano kombe la Shirikisho inafanyika leo jijini Cairo, Misri.
Timu 16 zilizofuzu makundi ligi ya mabingwa zitapangwa katika makundi manne ya timu nne nne wakati nyingine 16 zilizotolewa raundi ya kwanza ligi ya mabingwa zitapangiwa wapinzani kutoka timu 16 zilizofuzu raundi ya kwanza kombe la Shirikisho ili kupata timu zitakazotinga makundi, kombe la Shirikisho.
Yanga, mabingwa wa Tanzania ni miongoni mwa timu ambazo leo zitapangiwa mpinzani wake katika jitihada za kufuzu hatua ya makundi, kombe la Shirikisho.
Mchezo wa kwanza wa mtoano utapigwa kati ya April 06-08 na marudiano yakitarajiwa kuwa siku 10 baadae.

ADVERTISE HERE