Mabasi 50 kuwapeleka Wananchi Rwanda

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Sep 2023
Mabasi 50 kuwapeleka Wananchi Rwanda

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema mpaka sasa mabasi 50 yamethibitishwa yatasafirisha mashabiki wa Yanga nchini Rwanda kushuhudia mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa dhidi ya Al Merrikh

Aidha Kamwe amesema msafara wa mashabiki unaoanzia jijini Dar es salaam utaondoka nchini Alfajiri ya kuamkia kesho Alhamisi

"Mpaka wakati tunafunga zoezi la kuandikisha mashabiki wanaosafiri Rwanda, mabasi 50 nchi nzima yatasafirisha mashabiki nchini Rwanda"

"Kwa msafara unaoanzia safari Dar es salaam wafahamu kuwa muda wa safari ni saa 9 usiku wa kuamkia kesho Alhamisi"

"Kila mwananchi anayesafiri kwenda Rwanda ahakikishe ana nyaraka muhimu zitakazomruhusu kuingia Rwanda, tutafanya ukaguzi kabla ya kuanza safari ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza," alisema Kamwe

Viingilio vya mchezo huo utakaopigwa Jumamosi, Septemba 16 tayari vimetangazwa ambapo tiketi zinapatikana mtandaoni

VIP ni Tsh 104,000/-, Daraja la kati ni Tsh 52,000/- na Kawaida ni Tsh 20,900/-

Kamwe amewahakikishia mashabiki wote wanaosafiri nchini Rwanda wataingia uwanjani kushuhudia mchezo huo akikanusha uvumi kuwa Al Merrikh hawakuwa na mpango wa kuruhusu mashabiki

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’