Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga jioni ya leo wataondoka Tanzania kuelekea Rwanda wanakokabiliwa na mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Keshokutwa Jumamosi, Septemba 16 Yanga itashuka uwanja wa Pele, Kigali kuwakabili wenyeji wao Al Merrikh katika mchezo wa mkondo wa kwanza
Msafara wa mashabiki tayari umeondoka nchini kuelekea Rwanda ambapo takribani mabasi 50 yanawapeleka Wananchi Rwanda kuipa sapoti timu yao katika mchezo ambao Yanga imepania kusaka ushindi ugenini
Leo Yanga itasafiri bila ya nahodha wake Bakari Nondo Mwamnyeto ambaye amepewa ruhusa na Kocha Miguel Gamondi kwenda kushughulikia matatizo ya kifamilia
Hata hivyo Yanga ina utajiri mkubwa katika eneo la walinzi wa kati ambapo Ibrahim Bacca, Dickson Job na Gift Fred wote wako fit
Yanga inatarajiwa kupata mapokezi makubwa Rwanda, baadhi ya nyota wa zamani wa Yanga Haruna Niyonzima, Patrick Sibomana wakitoa hamasa kwa Wanyarwanda kuiunga mkono Yanga