Kazi ni moja leo, ushindi dhidi ya Al Merrikh

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Sep 2023
Kazi ni moja leo, ushindi dhidi ya Al Merrikh

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema wachezaji leo wana kazi moja tu, kuwapa furaha mashabiki wao katika mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya Al Merrikh

Hersi amesema Yanga haiko Rwanda kutalii, bali iko kwa ajili ya kusaka ushindi

Hersi amesema mashabiki wa Yanga waliobaki Tanzania kila mmoja kwa imani yake waendelee kuiombea timu uongozi ukiahidi leo itakuwa siku ya furaha kwao

"Yanga hatujaja hapa kufanya utalii, tumekuja kutafuta ushindi. Wapo watu wanaoweza kuomba dua ili tushinde, wafanye hivyo. Viongozi tupo kuhakikisha wachezaji wanatoa damu na jasho ili timu ishinde"

"Tunafahamu wachezaji siku hizi wanataka 'mzigo' ili wakimaliza shughuli uwanjani mifuko yao icheke. Tumejipanga na kila kitu kiko sawa, jukumu lao ni moja, kupambana uwanjani"

"Lakini pia tumesajili kikosi imara ili kitupe matokeo, haya mengine yote hayawezi kufanya kazi kama una timu mbovu. Chini ya uongozi wangu Yanga itaendelea kupanda tu! Mimi kama Rais wa klabu hii nawaambia hatuwezi kufeli," alisema Hersi

Muda wa mchezo ni saa 9 Alasiri kwa saa za Rwanda ambapo Tanzania ni saa 10 jioni

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
40m ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
4h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
23h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’