Alama tulioacha Rwanda haitafutika - Arafat

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Sep 2023
Alama tulioacha Rwanda haitafutika - Arafat

Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amewapongeza Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo waliosafiri kwa wingi nchini Rwanda kuishangilia timu yao katika mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Al Merrikh

Mchezo huo uliopigwa uwanja wa Pele, uliishuhudia Wananchi wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya makundi

Arafat amesema Yanga imeonyesha kwa vitendo kuwa ndio klabu kongwe yenye mashabiki wengi zaidi Tanzania

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Arafat ameandika ujumbe huu;

Yanga imeendelea kuthibitisha ukubwa wake ndani na nje ya nchi! Watu wa Rwanda wameshuhudia kwa vitendo kuwa sisi ndio timu kongwe na kubwa zaidi nchini, timu yenye mashabiki wengi, timu yenye mataji mengi.

"Alama tuliyoiacha Kigali Pele Stadium itaendelea kukumbukwa na haitofutika vizazi na vizazi! Wananchi tulikuwa ugenini kikanuni tu,lakini kwa namba ya mashabiki uwanjani tulikuwa wenyeji wa mchezo.

Nikiwa sehemu ya uongozi wa timu yetu pendwa, nachukua fursa hii kuwashukuru na kuwapongeza wanachama na mashabiki mliojitoa kwa hali na mali kwa kusafiri kutoka maeneo tofauti hadi Kigali, Rwanda kushangilia timu yetu.

Kwa namna moja au nyingine ushindi dhidi ya Al Merrikh umetokana na wingi wenu uwanjani na kusababisha deni kubwa kwa wachezaji na benchi la ufundi kuhakikisha mnapata furaha ambayo mmeifuata umbali mrefu kutoka nyumbani.

Zaidi ya mabasi 80 kutoka Tanzania yamebeba mashabiki wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 1,500! Wenyeji wamekiri jambo hili hawajawahi kuliona kwa timu ya kigeni kuwa na wingi wa mashabiki kwa kiasi hiki.

Kwa kipekee kabisa niwashukuru watu wa Rwanda kwa mapokezi na ukarimu wao kwetu. Bila shaka wote mliosafiri kutoka nyumbani Tanzania mmefurahia kuwa Kigali na mmejisikia mpo nyumbani.

Mwisho niwatakie safari njema Wananchi wote mnaosafiri kutoka Kigali, Rwanda kurejea nyumbani Tanzania, mfike salama.

KIGALI TAMU, WANANCHI TUTARUDI TENA!!"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’