Hersi aishukuru Rwanda

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Sep 2023
Hersi aishukuru Rwanda

Rais wa Yanga SC, Hersi Said ameishukuru nchi ya Rwanda ambayo iliwapokea na kuwahakikishia usalama Wanayanga waliosafiri kwa mamia kushuhudia mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji wao Al Merrikh ya Sudan

Pamoja na Yanga kuwa ugenini ndani ya ardhi inayoongozwa na Rais Paul Kagame, lakini ni kama ilikuwa nyumbani tu kutokana idadi kubwa ya mashabiki wao kuijaza Kigali na hata mapokezi waliyoyapata kutoka kwa wenyeji wao

Hersi ambaye kabla ya mchezo alimkabidhi Waziri wa Michezo wa Rwanda Aurore Mimosa Munyangaju jezi maalum ya Rais Kagame, amesema Yanga ilikuwa na wakati mzuri Rwanda na inashukuru kwa ukarimu waliopewa

"Tunashukuru kwa mapokezi tuliyopata hapa Rwanda, kwangu ilikuwa heshima kukabidhi jezi ya Yanga kwa Mheshimiwa Waziri wa Michezo wa Rwanda ikiwa ni zawadi maalumu kwa Mheshimiwa Rais Paul Kagame," alisema Hersi

Aidha Hersi amewashukuru Wanachama na Mashabiki wa Yanga waliosafiri kwa wingi Rwanda kwenda kuishangilia timu yao

Hersi amesema wingi wa Wananchi waliosafiri ni ishara ya imani kubwa ambayo Wananchi wameuoa uongozi wake na watahakikisha wanaendelea kuipambania nembo ya klabu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’