Ni zamu ya Namungo Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Sep 2023
Ni zamu ya Namungo Fc

Jana kikosi cha Yanga kilirejea mazoezi Avic Town na leo vijana wa Miguel Gamondi wanakamilisha maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc

Mchezo huo utapigwa kesho Jumatano katika uwanja wa Azam Complex

Baada ya ushindi wa mabao 5-0 katika mechi dhidi ya KMC na JKT Tanzania, Yanga imepania kuendeleza ubabe wake katika mchezo huo

Kabla ya msimu uliopita, Namungo Fc ilikuwa moja ya timu ngumu ambazo ziliwapa Wananchi wakati mgumu kwenye ligi

Hata hivyo msimu uliopita Namungo ilipoteza mechi zote mbili za ligi kuu dhidi ya Yanga na msimu huu pengine watakuwa na kazi ngumu zaidi mbele ya kikosi cha Gamondi

Ni mechi inayowakutanisha Wananchi na aliyekuwa kocha wao msaidizi Cedric Kaze ambaye kwa sasa ni mkufunzi wa Namungo

Wananchi wako tayari na wamemkaribisha Kaze Azam Complex wakimtahadharisha kuwa asije kichwa kichwa Chamazi, kwani kuna mnara wa 5G umesimikwa!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
45m ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
12h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
16h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
20h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
21h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’