Gamondi alia na uchovu Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Sep 2023
Gamondi alia na uchovu Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema ushindi dhidi ya Namungo Fc yalikuwa matokeo muhimu zaidi licha ya kuwa hakufurahishwa na vile timu yake ilicheza

Aidha Gamondi amebainisha kuwa kimbinu haikuwa rahisi kuipenya ngome ya Namungo Fc ambayo wachezaji 10 walikuwa nyuma ya mpira (walipaki basi)

"Nafikiri ushindi ndio matokeo muhimu kwetu lakini kwa ujumla sikufurahishwa na jinsi tulicheza. Nafahamu kuna mechi tutahitaji ushindi zaidi kuliko kucheza vizuri, hii inaweza kuwa mojawapo"

"Tulikosa umakini kwenye kumalizia lakini pia wachezaji walikuwa na haraka na kufanya maamuzi ambayo hayakuwa sahihi. Wapinzani wetu pia hawakuja kucheza mpira, walitumia kila mbinu ya kupoteza muda na bahati mbaya hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi yao"

"Yawezekana uchovu ulichangia kwa wachezaji wangu kukosa ubora wao kwani tumetoka kucheza mechi ngumu siku ya Jumamosi lakini nafurahi tumeweza kushinda," alisema Gamondi

Bao pekee la Yanga katika mchezo huo lilifungwa Mudathir Yahya aliyemalizia krosi ya chini kutoka kwa Yao

Shambulizi lilianzia kwa Jesus Moloko aliyempasia Aziz Ki ambaye alimpenyezea pasi Yao aliyemaliza uwanja kabla ya kupiga krosi ya chini

Ushindi huo umeirudisha Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 9 na mabao 11 ya kufunga pasipo kuruhusu bao lolote

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’