Maxi Mpia Nzengeli alibeba hamasa ya mchezo wa hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya Asas Fc ambao ulipigwa uwanja wa Azam Complex na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 5-1
Kitengo cha Hamasa cha Yanga chini ya Meneja wa Habari na Mahusiano Ali Kamwe msimu huu wamekuja na utaratibu tofauti katika mechi za Kimataifa ambazo Yanga inacheza nyumbani
Kila mechi ya nyumbani itatumika 'ku-brand' mchezaji mmoja lengo likiwa kuongeza hamasa pamoja na kuwaweka karibu wachezaji na mashabiki wao
Kamwe amewataka Wananchi kuchagua mchezaji ambaye wangependa abebe hamasa ya mchezo wa marudiano dhidi ya Al Merrikh ambao utapigwa Septemba 30 katika uwanja wa Azam Complex
Yanga inahitaji kushinda mchezo huo au hata matokeo ya sare ili kutinga hatua ya makundi
Wananchi walichomekea katika mchezo dhidi ya Asas Fc, sasa kipi kitafanyika katika mchezo dhidi ya Al Merrikh, Wananchi mtaamua!