Ubora wa Yanga unaanzia hapa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
28 Sep 2023
Ubora wa Yanga unaanzia hapa

Wakati makocha wengine wakikuna vichwa jinsi ya kuwatumia wachezaji, hali ni tofauti kwa Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi kwani licha ya kukabidhiwa kikosi msimu huu tayari asilimia 99 ya nyota wote 26 wamecheza michuano mbalimbali

Yanga imecheza mechi tisa kwenye mashindano mbalimbali ikiwa ni pamoja na mchezo mmoja wa wiki ya Mwananchi ambao ulikuwa maalumu kwa ajili ya kutambulisha kikosi cha msimu huu.

Katika mechi tisa, timu hiyo imefunga mabao 23 ikiruhusu nyavu zake kutikiswa mara moja ambapo ilianza dhidi ya Kaizer Chiefs na kushinda bao 1-0, dhidi ya Azam FC kwenye Ngao ya Jamii ikashinda 2-0, Ligi ya Mabingwa hatua ya awali na Asas FC ilishinda mabao 2-0 na ule wa marudiano ikashinda 5-1

Mechi za ligi ilianza na KMC ikaibuka na ushindi wa mabao 5-0, JKT Tanzania 5-0 na dhidi ya Namungo bao 1-0 huku ikiifunga Al Merreikh mabao 2-0.

Ushindi wa Yanga katika mechi zote hizo umechangiwa na kikosi chote kutokana na kocha Gamondi kutoa nafasi kwa kila mchezaji, huku kipa Abuutwalib Mshery akiwa ni pekee aliyekosa nafasi ya kucheza kutokana na kutoka kuuguza majeraha.

Wakati mastaa hao wakihusika kasoro Mshery, kuna baadhi ya wachezaji licha ya kupata nafasi ya kucheza kwenye Wiki ya Mwananchi, Ngao ya Jamii, Ligi ya Mabingwa, wapo waliokosa nafasi ya kucheza mechi za ligi ambao kati ya 26 ni watatu tu.

Yanga tayari imecheza mechi tatu za ligi ikikusanya pointi tisa na mabao 11, huku nyavu zake zikiwa hazijatikishwa hata mara moja na mastaa ambao hawajahusika kwenye ushindi huo ni Gift Fredy, Mahlatsi Makudubela ‘Scudu’, Chrispin Ngushi na Kibwana Shomari ambaye alikuwa panga pangua kikosini msimu uliopita chini ya Nasreddine Nabi na Salum Abubakar ‘Sure Boy’.

Wakati mastaa hao wakikosa nafasi mabeki Job na Yao wanaonekana kufunika zaidi kutokana na kutumika kwa dakika nyingi zaidi ya wengine huku nahodha Bakari Mwanyeto na kiungo Jonas Mkude wakitumika kwa dakika chache zaidi kwenye ligi wakicheza dakika saba katika mechi moja kati ya tatu.

Yao na Job kwenye mechi tatu za ligi wametumika kwa dakika 270 baada ya kucheza mechi zote kwa dakika 90 wakati wawili hao wakicheza dakika hizo, Ibrahim Abdallah ‘Bacca’ amefuata kwa kucheza dakika 264, Khalid Aucho 253, Stephane Aziz Ki 246, Keneddy Musonda 232, Mudathir Yahya 203, Maxi Nzengeli 197, Dickson Kibabage 185, Djigui Diarra 180, Pacôme Zouzoua 157, Jesus Moloko 102, Clement Mzize 98, Metacha Mnata 90, Konkoni 85, Joyce Lomalisa 59, Zawadi Mauya 28 na Farid Mussa 26.

Gamondi amesema kikosi chake kipo fiti na wachezaji wengi wana uwezo sawa ndio maana amekuwa akitoa nafasi kwa mastaa wote.

"Nafurahi kufanya kazi na Yanga ina wachezaji wengi wazuri na wote wana uchu wa mafanikio hiyo ndio inaweza kuwa siri ya matokeo mazuri ambayo tumekuwa tukiyapata ndani ya uwanja"

"Hatuna mchezaji tegemezi kila mchezaji anatumika kutokana na ushawishi wake mazoezini, kuhusu uwezo kwa asilimia kubwa wote wana uwezo sawa kinachotofautisha ni aina ya uchezaji na kila mmoja anatumika kutokana na aina ya mpinzani tunayekutana naye," alisema Gamondi

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE →
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE →
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE →
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE →
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE →
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →