Hatufanyi tena makosa uwanja wa Taifa - Nsajigwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Mar 2018
Hatufanyi tena makosa uwanja wa Taifa - Nsajigwa
Wawakilishi pekee wa Tanzania waliobakia kwenye mashindano ya kimataifa, Yanga, wameshaanza mikakati ya kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga imeanza kujifua jana kujiandaa na mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Singida United utakaopigwa kwenye uwanja wa Namfua April 01.

Baada ya mchezo huo Yanga itarejea uwanja wa Taifa kuivaa Welayta kwenye mchezo wa kwanza wa mtoano kombe la Shirikisho kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi.

Mchezo huo unatarajia kupigwa kati ya April 06,07 na 08.

Yanga itawafuata wapinzani wao kwa ajili ya mechi ya marudiano ya hatua hiyo ya mtoano kati ya Aprili 17 na 18 huko Addis Ababa, Ethiopia.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, amesema ili wawe na uhakika wa kusonga mbele ni lazima wahakikishe wanapata matokeo mazuri katika uwanja wa nyumbani na hawataki kuona wanarudia makosa waliyofanya kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.<

Nsajigwa amesema changamoto waliyokuwa nayo ni kujiandaa vyema kwa ajili ya mechi hiyo huku vile vile wakitakiwa kupambana ili kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara wanaoushikilia.

"Kama nilivyosema jana (juzi), fainali yetu, hesabu zetu tunatakiwa kuzifunga hapa nyumbani, unapofanya vizuri nyumbani au katika mechi ya kwanza, unajiweka kwenye mazingira mazuri ya kusonga mbele, hiyo ndiyo siri ya mafanikio," alisema Nsajigwa.

Yanga imehamia kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa na mabingwa wa Botswana, Township Rollers kwa kichapo cha mabao 2-1 walichofungwa hapa nyumbani wakati Welayta Dicha yenyewe imeiondoa Zamalek ya Misri kwa penalti 4-3 baada ya kufungana mabao 3-3.

Wapinzani hao wa Yanga ambao ni mabingwa wa Kombe la FA huko Ethiopia mwaka jana, wako katika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi ya ndani wakiwa na pointi 19 baada ya kushinda mechi tano na kutoka sare michezo minne wakati vinara ni Dedebit wenye pointi 29.

Mshindi wa jumla kati ya Yanga na Welayta Dicha atatinga hatua ya makundi ya mashindano hayo yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf).

Mara ya mwisho Yanga kutinga hatua ya makundi ilikuwa ni mwaka 2016, walipopangwa kundi moja na Medeama ya Ghana, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Mo Bejaia ya Algeria.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’