Mshambuliaji wa Yanga Hafiz Konkoni amewaahidi Wananchi kuwa ataendelea kupambana ili kuhakikisha anapata nafasi ya kuonekana dimbani mara kwa mara
Konkoni amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi mbele na Clement Mzize na Kennedy Musonda ambao wanaonekana kuwa chaguo la kwanza
Baada ya kukosekana uwanjani kwa takribani mechi tatu, Konkoni alipata nafasi kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Geita Gold, mchezo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-0
Dakika alizopata kwenye kipindi cha pili zilifufua matumaini pengine anaweza kupata nafasi zaidi kama ataendelea kupambana
"Wakati wa mungu ndio wakati sahihi hakuna mafanikio yanayokuja kirahisi, nitaendelea kupambana na kuwa mvumilivu kwani naamini nitafanikiwa," aliandika Konkoni kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema mchezo huo hakuwa fit kwa asilimia 100 kulinganisha na wenzake kwa kuwa alichelewa kujiunga na timu
Aidha Konkoni alipata majeraha ambayo yalimuweka nje kwa takribani wiki moja, amerejea tena kupigania nafasi yake
Msimu huu Konkoni amefunga mabao mawili, akipachika bao katika ligi kuu na ligi ya mabingwa