Aziz Ki amepania 'mpaka waseme'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Oct 2023
Aziz Ki amepania 'mpaka waseme'

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki msimu huu amepania kuwaziba midomo wale wote waliokuwa wanahoji ubora wake msimu uliopita

Achana na idadi ya mabao matatu aliyofunga kwenye ligi pamoja na pasi yake moja ya bao, Aziz Ki ndiye kiungo mshambuliaji mwenye takwimu bora zaidi kulinganisha na wachezaji wengine wanaocheza katika nafasi yake

Nyota huyo raia wa Burkina Faso, amepiga jumla ya mashuti 11 yaliyolenga lango, matatu yakijaa kambani

Ametengeneza nafasi 7 huku akipiga pasi muhimu 10 za kuwafungua wapinzani

Ki ameingia kwenye eneo la wapinzani mara nyingi akigusa mipira mara 15 katika eneo hilo

Katika kikosi cha kocha Miguel Gamondi, Aziz Ki ni mchezaji mwenye uhakika wa kuanza katika kila mechi

Kwa hakika Aziz Ki atakuwa 'funguo' muhimu kwa Yanga kwenye hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
10h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
14h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
19h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
22h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’