Kazini kwa Konkoni 'kuna kazi'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Oct 2023
Kazini kwa Konkoni 'kuna kazi'

Mshambuliaji Hafiz Konkoni bado hajaweza kuwapa raha mashabiki wa Yanga ambao ni wazi wanaendelea kumvumilia kwa sababu hana muda mrefu kikosini

Konkoni alisajiliwa kama mbadala wa Fiston Mayele aliyetimkia Pyramids ya Misri katika dirisha la usajili lililopita

Mayele alijijengea heshima kubwa Yanga, alikuwa mchezaji kipenzi cha mashabiki kwani alifanya vyema kazi ya kuziadhibu timu pinzani

Konkoni hajawa na mwanzo mzuri, mpaka sasa amefunga mabao mawili akifunga kwenye ligi kuu (dhidi ya KMC) na ligi ya mabingwa (dhidi ya Asas Fc)

Wakati mwingine imekuwa sio rahisi kwake kupata nafasi ya kucheza mbele ya Clement Mzize na Kennedy Musonda pamoja na kuwa zipo nyakati alikosekana kwa sababu alikuwa majeruhi

Konkoni alirejea tena kikosini katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Geita Gold uliopigwa jijini Mwanza kabla ya mapumziko ya FIFA

Katika mchezo huo ambao Yanga ilishinda mabao 3-0, aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mzize anayeonekana kuwa mshambuliaji chaguo la kwanza kwa sasa

Ni wazi mshambuliaji huyo raia wa Ghana ana kazi ya kuwashawishi Wananchi lakini kazi yake inaonekana ni kubwa zaidi kwa sababu amechukua nafasi ya mchezaji ambaye alifanya mambo makubwa sana

Konkoni ni mshambuliaji ambaye yawezekana bado hajafanikiwa kuingia kwenye mbinu za Kocha Miguel Gamondi kwani asili yake ni mshambuliaji anayependa kusimama kwenye eneo la hatari la timu pinzani

Master Gamondi yeye aanapendelea zaidi mshambuliaji ambaye anafanya majukumu zaidi ya kufunga awapo uwanjani

Mzize anaonekana kuwazidi wenzake kwa sababu anaposimama pale mbele, pia anaongoza 'pressing' kuhakikisha hawapi utulivu walinzi wa timu pinzani katika kuanzisha mipira kutokea nyuma

Pengine Konkoni nae anapaswa kubadilika ili kwendana na mahitaji ya kimbinu ya Gamondi kwani kwa umbile lake ziko mechi ambazo anafaa zaidi kutumika mbele ya Mzize na Musonda

Ni mshambuliaji asiye na mambo mengi uwanjani, ana nguvu na sio rahisi kumnyang'anya mpira anapouweka mguuni

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
10h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
14h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
15h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
15h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’