Nani anaanza, nani anasubiri dhidi ya Azam Fc leo?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Oct 2023
Nani anaanza, nani anasubiri dhidi ya Azam Fc leo?

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi leo anahitaji kuanza na silaha zake zote ili kuhakikisha ushindi unapatikana katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa saa 12:30 jioni

Habari njema kwa Gamondi ni kuwa hakuna mchezaji wa kikosi cha kwanza ambaye ni majeruhi

Farid Mussa aliyekuwa nje kwa muda mrefu nae alisharejea mazoezini kujiandaa na mchezo huo

Stephane Aziz Ki alikuwa mchezaji wa mwisho kurejea kutoka kwenye majukumu ya timu ya Taifa

Alitua Ijumaa usiku hivyo alifanya mazoezi siku za Jumamosi na Jumapili, ni wazi leo atakuwa miongoni mwa wanaume 11 watakaoanza kuikabili Azam Fc

Hakuna shaka golini Djigui Diarra ataanza wakati walinzi wa pembeni huenda wakaanza Yao Yao na Joyce Lomalisa

Walinzi wa kati hapa Gamondi ataamua aanze na pacha ipi maana Ibrahim Bacca, nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto, Dickson Job na hata Gift Fred wote wako fit

Khalid Aucho, Mudathir Yahya wanaweza kuendelea kuwa chaguo la kwanza kwenye eneo la kiungo

Wakati Maxi Nzengeli, Stephane Aziz Ki na Pacome Zouzoua (MAP) wanatarajiwa kuongoza eneo la viungo washambuliaji

Max, Aziz na Pacome ndio vinara wa kupachika mabao kwenye kikosi cha Yanga wakiwa wamefunga mabao tisa (mabao matatu kila mmoja)

Katika safu ya ushambuliaji Clement Mzize, Kennedy Musonda na Hafiz Konkoni wote wako 'fit' lakini ni mmoja tu ambaye atakuwa na nafasi ya kuanza

Jambo muhimu kwa Yanga leo ni msako wa alama tatu katika mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’