Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi jana alikuwepo uwanja wa Benjamin Mkapa kushuhudia mchezo wa Simba dhidi ya Ihefu Fc ikiwa ni sehemu ya makakati wake kuhakikisha mchezo unaofuata dhidi ya Simba alama tatu zinabaki Jangwani
Gamondi pia alishuhudia mchezo ambao Simba walicheza na Al Ahly katika michuano ya AFL katika uwanja huo wa Benjamin Mkapa
Yanga imeanza maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa Novemba 05, dimba la Mkapa saa 11 jioni
Huu ni mchezo muhimu kwa Yanga kushinda ili kujihakikishia kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya NBC na pengine kuwa mwanzo wa safari ya kutetea ubingwa kwa msimu wa tatu mfululizo
Gamondi ana kumbukumbu ya kile kilichotokea mkoani Tanga kwenye Ngao ya Jamii, Yanga ikipoteza kwa mikwaju ya penati baada ya suluhu ya bila kufungana
Yanga ilitawala mchezo lakini haikutumia nafasi nyingi walizotengeneza licha ya kuwa walifunga mabao mawili yaliyokataliwa na waamuzi kutokana wafungaji kuwa wameotea
Itakuwa derby ya kwanza ya Kariakoo msimu huu Simba wakiwa wenyeji wa mchezo huo
Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi na Meneja wa timu hiyo Walter Haryson wametinga katika Uwanja wa Mkapa kutazama mchezo wa Ligi kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Ihefu.