Simba walimsahau huyu mwenye 'blichi'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Nov 2023
Simba walimsahau huyu mwenye 'blichi'

Unakumbuka mchezo uliopita dhidi ya Azam Fc ambao ulipigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 3-2?

Kocha wa Azam Fc Yousuph Dabo katika moja ya clip za video alionekana akiwaelekeza wachezaji wake wamkabe mchezaji mwenye nywele zenye rangi (alionyesha kwa vitendo)

Alimaanisha Pacome Zouzoua 'Profesa' kwani aliwaweka katika wakati mgumu kila aliposhika mpira

Huyu Pacome hakuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Ivory Coast msimu uliopita kwa bahati mbaya

Pengine katika mchezo dhidi ya Simba jana, Pacome alistahili kuondoka na tuzo ya mchezaji bora wa mechi

Wengi walitamani mkwaju wa penati uliopatikana kwenye dakika ya 86 angepiga Maxi Nzengeli mwenyewe ili kuifikia rekodi ya Mzee Abdallah Kibadeni mchezaji pekee aliyewahi kufunga hat-trik katika mchezo wa derby

Mkwaju huo wa penati akapewa Pacome, naamini wachezaji wenzake walimpa kwa heshima ya kiwango bora alichoonyesha kwenye mchezo huo

Msimu huu Pacome amefunga mabao manne na kutoa pasi moja ya bao kwenye ligi kuu

MAP imeendelea kun'gara sasa ikihusika katika mabao 18 ya Yanga msimu huu

Max aliweka kambani mabao mawili jana akifikisha mabao saba sawa na Stephane Aziz Ki aliyefunga bao moja na kutoa assist moja

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’