Baada ya kushuhudia dabi ya Soweto kati ya Kaizer Chiefs dhidi ya Orlando Pirates iliyomalizika kwa Pirates kuibuka na ushindi wa bao 1-0, usiku Rais wa Yanga Injinia Hersi Said akahudhuria hafla maalum ya kumkaribisha Afrika Kusini Rais wa FIFA, Gianni Infantino
Hersi akapata nafasi ya kuzungumza na Infantino sambamba na Rais wa CAF, Patrice Motsepe
Leo mchezo wa pili wa fainali ya African Football League kati ya Mamelodi Sundowns dhidi ya Wydad unapigwa huko Afrika Kusini, Hersi ni miongoni mwa wageni walioalikwa kushuhudia mchezo huo
Yanga inatarajiwa kushiriki michuano ya African Football League msimu ujao
Kwenye Hafla maalum inayoendelea hapa Johannesburg, Afrika Kusini Rais wa Young Africans Sports Club, Eng Hersi Said amekutana na Rais wa FIFA Gianni Infantino akiwa na mwenyeji wake Rais wa CAF Patrice Motsepe
— Young Africans SC (@YoungAfricansSC) November 11, 2023
Miongoni mwa mambo ambayo Rais wa FIFA Gianni Infantino aliyauliza⦠pic.twitter.com/hPxx5rDTdP