Wakati Yanga ikitarajiwa kukata rufaa kupinga adhabu ya kufungiwa mechi tatu aliyopewa kiungo Khalid Aucho, Kocha Miguel Gamondi atahitaji kuziba pengo lake katika mechi tatu ambazo atakosekana kwenye Ligi
Ifahamike adhabu ya Aucho inahusu mechi za Ligi na FA tu, atakuwa sehemu ya kikosi katika mechi zinazofuata kwenye ligi ya mabingwa
Aucho anatarajiwa kukosa mechi zinazofuata kwenye ligi dhidi ya Mtibwa Sugar, Tabora United na Kagera Sugar
Pengine hii inaweza kuwa nafasi kwa baadhi ya wachezaji kurejea kikosini, Salum Abubakar 'Sure Boy', Jonas Mkude na Zawadi Mauya
Mauya ndiye aliyetumika zaidi kati yao akifuatiwa na Mkude wakati upande wa Sureboy nafasi yake imekuwa finyu msimu huu
Lakini kukosekana kwa Aucho ni wazi itakuwa nafasi kwa Sureboy ambaye msimu uliopita alikuwa mmoja wa wachezaji muhimu kwenye kikosi cha Nasreddine Nabi, kumshawishi Gamondi ampatie nafasi zaidi