Mzize tayari kwa majukumu makubwa Algeria

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Nov 2023
Mzize tayari kwa majukumu makubwa Algeria

Kwa sasa mshambuliaji kinda Clement Mzize amekomaa na tayari kupewa majukumu makubwa katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika kuanzia hatua ya makundi

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi hana la zaidi ya kumuamini Mzize kwani amedhihirisha, uwezo wa kuongoza safu ya ushambuliaji anao

Mzize alikuwa kinara wa kupachika mabao kwenye hatua za awali ligi ya mabingwa akifunga mabao matatu

Alifunga bao moja katika mchezo dhidi ya Asas Fc pia akafunga katika mechi zote mbili dhidi ya Al Merrikh

Kiwango bora alichoonyesha katika mechi mbili zilizopita, kinamuweka katika nafasi nzuri ya kuanza mchezo dhidi ya CR Belouizdad siku ya Ijumaa mbele ya Kennedy Musonda na Hafiz Konkoni ambaye imekuwa ngumu kwake kupenya kwenye kikosi cha kwanza

Akiingia kutokea benchi, Mzize alitoa pasi mbili za mabao katika ushindi wa mabao 5-1 ambao Yanga waliupata dhidi ya watani zao Simba Novemba 05 na pia akafunga bao pekee la ushindi katika mchezo dhidi ya Coastal Union uliopigwa Tanga Novemba 08

Awapo uwanjani, Mzize anakuwa na muunganiko mzuri na viungo wa washambuliaji Pacome Zouzoua, Stephane Aziz Ki na Max Nzengeli (MAP) na mara nyingi amehusika katika upatikanaji wa mabao kwenye mechi za karibuni

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’