Bacca Day yazinduliwa Zanzibar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Nov 2023
Bacca Day yazinduliwa Zanzibar

Kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Al Ahly ambao utapigwa Jumamosi Disemba 02, leo Yanga imefanya tukio la aina yake visiwani Zanzibar kwa kuzindua siku ya BACCA DAY

Akizungumza katika hafla maalum ya uzinduzi wa tukio hilo, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema ni mwendelezo wa utamaduni wa Yanga kuwapa thamani wachezaji wao lakini safari hii tukio hili limekwenda mbali zaidi kwa ajili ya manufaa ya nchi

"Tumekuwa na Maxi Day, Aziz Ki Day, wote walipata nafasi ya kutengenezewa thamani katika mechi zilizopita. Tumekutana hapa Zanzibar leo kwa ajili ya mchezaji wetu Ibrahim Bacca"

"Yanga ilimpa nafasi Bacca ya kuonyesha kipaji chake mazoezini na kwa utulivu na uvumilivu ilimchukua miezi kadhaa mpaka kuaminiwa kwenye kikosi cha kwanza"

"Leo tumekutana kuzindua Bacca Day ambayo kilele chake ni Disemba 02 pale uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly"

"Tukio hili limekwenda mbali zaidi sio tu kumpa thamani mchezaji wetu, Taasisi kubwa mbili hapa Zanzibar, ZRA na ZIPA zilipelekewa mapendekezo jinsi gani tukio hili linaweza kuwaongezea thamani"

"Taasisi hizo zimeweka fedha kwa ajili ya kudhamini Bacca Day kila Taasisi ikitoa Tsh Milioni 20. Nawapongeza ZIPA na ZRA kwa kuona kwa kiasiΒ  gani Bacca day inaweza kutumika kuwatangaza"

"Leo natangaza rasmi kuzindua Wiki ya Bacca Day ambayo kilele chake ni Disemba 02 pale uwanja wa Benjamin Mkapa," alisema Hersi

Nae Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema Disemba 02 itakuwa siku maalum hivyo watakuwa na mtoko maalum

"Kama una msuli wako uliuweka ndani kwa muda mrefu basi Jumamosi ndio siku yake. Vaa jezi yako na msuli wako njoo uwanjani"

"Lakini pia kama una kanzu yako basi vaa njoo nayo siku hiyo kuja kuipa thamani Bacca Day"

"Kwa wale wenzetu wanaofanya kazi vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutambua Bacca ni mwajiriwa wa Jeshi (KMKM), basi waje uwanjani na magwanda yao katika siku hii," alisema kamwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
21h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
22h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’