Tunawaheshimu Al Ahly lakini hatuwaogopi - Job

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Nov 2023
Tunawaheshimu Al Ahly lakini hatuwaogopi - Job

Mlinzi wa kati ya Yanga Dickson Job amesema wanaendelea vyema na maandalizi kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly

Ni mtanange wa kukata na shoka, utapigwa Jumamosi, Disemba 02 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, muda wa mchezo ukiwa ni saa 1 usiku

Mchezo huo utaadhimisha Bacca Day ukiwa ni mchezo maalum kwa ajili ya kumthamini na kutambua mchango wa beki Ibrahim Bacca

Job amesema wanatambua Al Ahly ni mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwa ikiwa klabu bora barani Afrika kwa sasa. Watawaheshimu kutokana na mafanikio yao lakini hawawezi kuwaogopa kwa sababu kila timu itakuwa na wachezaji 11 uwanjani

Job amesema wanahitaji kuwapa furaha mashabiki wao kwa kushinda nyumbani hasa ikizingatiwa walipoteza mchezo uliopita dhidi ya CR Belouizdad

"Tunarudi kucheza dhidi ya timu bora Afrika na tunawaheshimu, ila hatuwezi kuwaogopa kwani mchezo ni dakika 90 na wachezaji wa pande zote wana uwezo mkubwa wa kucheza"

"Tutaongeza umakini wa kupata matokeo lakini pia kuhakikisha sisi kama mabeki hatuwapi nafasi wapinzani kufunga. Hatupo tayari kupoteza mara mbili hasa uwanja wa nyumbani" alisema Job

Yanga ilipoteza mchezo wa kwanza ugenini kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya CR Belouizdad hata hivyo ushindi dhidi ya Al Ahly utarejesha matumaini ya Yanga kuwania tiketi kutinga robo fainali ya michuano hiyo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
11h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
16h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
20h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’