Jumamosi ya wiki hii Disemba 02 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Yanga itakuwa mwenyeji wa Al Ahly katika mchezo wa raundi ya pili hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika
Hii ni mechi muhimu kwa Yanga kusaka ushindi ili kuweka hai matumaini ya kuwania nafasi ya kutinga robo fainali ya ligi ya mabingwa
Ni wazi hautakuwa mchezo mwepesi, Al Ahly ndio mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwa na msimu huu wameanza vyema kampeni ya kutetea taji lao wakiifunga Medeama mabao 3-0 katika mchezo uliopita
Jambo la uhakika ni kuwa mchezo huo utakuwa mgumu lakini Yanga haijawahi kuwa mnyonge mbele ya Al Ahly
Ukiangalia mechi nne zilizopita Yanga ilishinda mechi moja na Al Ahly kushinda mechi mbili huku mechi moja timu hizo zikitoka sare
Mwaka 2014 Yanga na Al Ahly zilikutana hatua ya mtoano ligi ya mabingwa Yanga ikishinda bao 1-0 nyumbani na Al Ahly kupata ushindi kama huo kwao na baadae Yanga kuondoshwa mashindanoni kupitia changamoto ya mikwaju ya penati
Mara ya mwisho kwa timu hizo kukutana kwenye ligi ya mabingwa ni mwaka 2016, mchezo wa kwanza uliopigwa Dar kumalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 na Al Ahly kushinda mabao 2-1 katika mchezo wa marudiano uliopigwa Misri
Yanga haijawahi kupoteza mchezo dhidi ya Al Ahly inapocheza nyumbani katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Wakati huu Yanga inaikaribisha tena Al Ahly kwa Mkapa ikiwa bora zaidi pengine kuliko wakati mwingine wowote
Baada ya kupoteza mchezo ulopita dhidi ya CR Belouizdad, Yanga inahitaji kushinda mchezo huu