Yanga kuifuata Singida United kibabe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Mar 2018
Yanga kuifuata Singida United kibabe
Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuifuata Singida United leo kwa ajili ya mchezo wa robo fainali kombe la FA (ASFC) utakaopigwa kwenye dimba la Namfua, keshokutwa April 01, 2018.

Yanga iliweka kambi mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo huo ambao mshindi atatinga nusu fainali kuukaribia ubingwa.

Timu hiyo inayonolewa na kocha George Lwandamina inakwenda Singida ikiwa na kikosi chake kamili kinachomjumuisha mshambuliaji Donald Ngoma aliyerejea kikosini baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu.

Hata hivyo Yanga itawakosa Ramadhani Kabwili, Maka Edward na Said Mussa ambao wako kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes ambapo kesho itashuka kwenye uwanja wa taifa kucheza na DR Congo katika mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu AFCON 2019.

Pia mshambuliaji Amissi Tambwe aliachwa jijini Dar es salaam licha ya kuwa amepona majeraha. Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema Tambwe alipewa program maalum ya mazoezi na ataungana na wenzake kujiandaa na mchezo dhidi ya Welayta Dicha.

Saleh amesema wachezaji wengine walio kambini mkoani Morogoro wako tayari kwa ajili ya mchezo huo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’