Kesho Jumatano Yanga inashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kumenyana na Medeama Fc katika mchezo wa nne wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika
Hii ni mechi muhimu kwa Yanga kushinda ili kuweka hai matumaini ya kufuzu robo fainali ya ligi ya mabingwa
Kimahesabu kama Yanga itapata ushindi mnono wa kuanzia mabao matatu, inaweza kutoka nafasi ya mwisho kundi D hadi kileleni mwa kundi kwani itafikisha alama tano kama ilivyo kwa Al Ahly
Mchezo kati ya CR Belouizdad dhidi ya Al Ahly umepigwa kalenda mpaka Al Ahly watakapomaliza kushiriki michuano ya FIFA ya klabu bingwa
Yanga itakuwa ikisaka ushindi wa kwanza dhidi ya Medeama ambayo katika mechi mbili zilizopita dhidi ya Yanga katika mashindano yote imekusanya alama nne
Mwaka 2016 Yanga ilikuwa kundi moja na Medeama Fc makundi ya kombe la Shirikisho, mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa ukimalizika kwa sare ya bao 1-1 na Medeama kushinda mabao 3-1 katika mchezo wa pili uliopigwa Ghana
Mchezo wa kwanza kwenye ligi ya mabingwa msimu huu ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 huko Ghana na kesho utakuwa mchezo wa pili baina ya timu hizo
Ni mechi ambayo Yanga inahitaji matokeo ya ushindi zaidi, matokeo tofauti yatafifisha matumaini ya Yanga kucheza robo fainali