Kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua ameendelea kuin'garisha Yanga katika michuano ya ligi ya mabingwa Afrika leo akifunga katika mchezo wa tatu mfululizo na kuisaidia Yanga kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Medeama
Pacome amefikisha mabao matatu sasa akiingia kwenye vita ya ufungaji bora akichuana na Sankara Karamoko wa Asec anayeongoza akiwa na mabao 4
Huu unaweza kuwa msimu bora sana kwa Pacome kwani mchango wake katika kikosi cha Yanga ni mkubwa
Pacome amejumuishwa katika kikosi cha awali cha timu ya Taifa ya Ivory Coast itakayoshiriki michuano ya Afcon 2024 inayoanza mwezi Januari huko Ivory Coast
Kwa hakika Pacome ni Zizou wa Afrika...!
ADVERTISE HERE