Licha ya kukosa muda wa kufanya maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tabora United, Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema wako mkoani Dodoma kuwania alama tatu muhimu dhidi ya Tabora United
Gamondi amesema wametoka kucheza mechi ya ligi ya mabingwa na ndani ya siku tatu wanakabiliwa na mchezo huo wa ligi kuu, hivyo wamekuwa na vipindi vya 'recovery' kurejesha utimamu wa miili ya wachezaji
"Kucheza kila baada ya siku tatu sio jambo rahisi, tumetoka kucheza mechi ya ligi ya mabingwa, kesho tutacheza hapa Dodoma na Jumanne tuna mchezo mwingine"
"Kuna uchovu na majeruhi kwa baadhi ya wachezaji lakini jambo muhimu ni kuwa tuko tayari kwa mchezo dhidi ya Tabora United"
"Tutarajie kuona mabadiliko kwa kulingana na aina ya mpinzani, tutawakosa wachezaji wawili Khalid Aucho anayetumikia adhabu na Joyce Lomalisa ambaye bado ni majeruhi lakini tuna wachezaji wengine ambao tunaweza kuwatumia katika nafasi zao," alisema Gamondi
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake mlinda lango Metacha Mnata amesema pamoja na ugumu wa ratiba wamejipanga kuhakikisha wanashinda mchezo huo
"Sio rahisi kwa sababu tunacheza mechi mfululizo lakini timu ina wachezaji 29 hivyo naamini benchi la ufundi watachagua wachezaji ambao wako tayari kwa mchezo lengo letu ni kushinda," alisema