Yanga inaweza kushiriki FIFA Club World Cup 2025 kama itaweza kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa msimu huu
FIFA imetoa nafasi nne kwa bara la Afrika na ikaweka vigezo namna ya kuzipata klabu hizo
Wamechukua mafanikio ya timu katika michuano ya ligi ya mabingwa kuanzia msimu wa 2020/21 hadi 2023/24 yaani msimu huu ambao bado bingwa hajajulikana
Nafasi mbili tayari zimechukuliwa Al Ahly na Wydad kwani katika kipindi hicho zimetwaa mataji ya ligi ya mabingwa
Nafasi mbili zilizobaki, moja itapatikana kwa kuangalia ranking za CAF katika kipindi husika na moja itachukuliwa na bingwa Ligi ya Mabingwa msimu huu
Hii inamaanisha kama Yanga itaweza kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa msimu huu, basi nayo itashiriki
Nafasi hii iko kwa timu zote 14 kati ya 16 ambazo zinashiriki hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa
Katika ranking, iliyo na nafasi zaidi ni Mamelodi Sundowns ambao mpaka sasa wamekusanya alama 81
Esperance ni ya pili ikiwa na alama 75. CR Belouzdad inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 59 huku Petro Atletico wakishika nafasi ya nne wakiwa na alama 49
Simba kutoka Tanzania ina alama 45 ikishika nafasi ya tano. Hivyo kama watataka kufuzu kupitia ranking watahitaji kukusanya alama nyingi kuzipita timu zilizo juu yake na wakati huohuo ikiziombea mabaya timu hizo zisikusanye alama zozote jambo ambalo kiuhalisia ni gumu