Nyota wa Yanga, Stephane Aziz KI, amepenya katika mchujo wa mwisho wa kocha Hubert Velud na sasa atakuwa miongoni mwa nyota 27 watakaoiwakilisha Burkina Faso katika fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) zitakazofanyika mwakani huko Ivory Coast
Kiwango bora ambacho amekionyesha katika kikosi cha Yanga msimu huu akifungia mabao 10 na kupiga pasi mbili za mwisho kwenye Ligi Kuu pamoja na kucheza mechi zote za Ligi ya Mabingwa Afrika kinaonekana kumkosha Velud ambaye ameamua kwenda naye Ivory Coast baada ya kuwapungua wachezaji 28 kutoka kwenye kikosi cha awali cha wachezaji 55
Kikosi cha mwisho cha Burkina Faso
Makipa: Herve Koffi, Hillel Konate, Kilian Nikiema na Sebastien Tou.
Mabeki: Issa Kabore, Steeve Yago, Issoufou Dayo, Nasser Djiga, Edmond Tapsoba, Abdoul Guiebre na Valentin Nouma.
Viungo: Blati Toure, Adama Guira, Dramane Salou, Ismaila Ouedraogo, Sacha Banse, Gustavo Sangare na Azik KI.
Washambuliaji: Bertrand Traore, Dango Ouattara, Hassane Bande, Mohamed Konate, Fessal Tapsoba na Cedric Badolo