Kuelekea michuano ya kombe la Mapinduzi, Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi anatarajia kuwapa mapumziko baadhi ya wachezaji ambao wametumika sana msimu huu
Kikosi cha Yanga kitaelekea Zanzibar Disemba 30 kushiriki michuano hiyo wakitarajiwa kusafiri na wachezaji wote ambao hawako kwenye majukumu ya timu za Taifa
Hii itakuwa nafasi kwa baadhi ya wachezaji ambao nafasi yao katika kikosi cha kwanza ilikuwa finyu
Hapa tunawazungumzia wachezaji kama Aboutwalib Mshery, Kibwana shomari, Salum Abubakar, Zawadi Mauya, Gift Fred, Jonas Mkude, Skudu, Denis Nkane, Crispine Ngushi na wengine
Max Nzengeli, Yao Kouassi, Khalid Aucho ni miongoni mwa wachezaji ambao huenda wakapewa mapumziko
Aidha Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amedokeza kuwa katika michuano hiyo zikaonekana sura mpya ikiwa pamoja na baadhi ya wachezaji kutoka timu ya vijana U20