Gamondi apiga hesabu kali Mapinduzi Cup

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Dec 2023
Gamondi apiga hesabu kali Mapinduzi Cup

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi anatarajiwa kuelekea Zanzibar akiwa na kikosi chake kamili kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi inayoanza kutimua vumbi leo

Gamondi amesema baada ya ligi kusimama, michuano hii ataitumia kuwaweka wachezaji wake katika ubora akifahamu baada ya mashindano ya Afcon kumalizika ratiba itakuwa ngumu

Yanga itaondoka nchini Jumamosi Disemba 30 ikiwa na wachezaji wote ambao hawatakuwa kwenye majukumu ya timu za Taifa

"Tunahitaji kutumia michuano hii ili tuendelee kujiimarisha. Nafahamu tutakuwa na ratiba ngumu baada ya michuano ya Afcon kumalizika"

"Ligi, FA na Ligi ya Mabingwa mashindano yote yatapaswa kumalizika katika kipindi cha miezi mitatu hadi minne"

"Hatuwezi kuwa na mapumziko kwa sababu lazima tujiandae vyema," alisema Gamondi

Yanga ilirejea mazoezini juzi kujiandaa na michuano hiyo huku ikiwakosa wachezaji 13 ambao walijumuishwa katika vikosi vya awali vya timu za Taifa kwa ajili ya Afcon 2023

Wachezaji Stephane Aziz Ki na Djigui Diarra tayari wamejumuishwa kweny vikosi vya mwisho vya timu Mataifa ya Burkina Faso na Mali

Hafiz Konkoni, Pacome Zouzoea, Metacha Mnata, Aboutwalib Mshery, Nickson Kibabage, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Hamad 'Bacca', Mudathiri Yahya na Clement Mzize bado wanasubiri mchujo wa mwisho katika mataifa yao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’